Psalms 19:4-6

4 aSauti yao imeenea duniani pote,
nayo maneno yao yameenea
hadi miisho ya ulimwengu.

Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,
5 blinafanana na bwana arusi
akitoka chumbani mwake,
kama shujaa afurahiavyo
kukamilisha kushindana kwake.
6 cHuchomoza upande mmoja wa mbingu,
na kufanya mzunguko wake
hadi upande mwingine.
Hakuna kilichojificha joto lake.
Copyright information for SwhNEN